Deuteronomy 30

Mafanikio Baada Ya Kumgeukia Bwana

1 aWakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popote Bwana Mwenyezi Mungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa, 2 bhapo wewe na watoto wako mtakapomrudia Bwana Mwenyezi Mungu wako, na kumtii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kulingana na kila kitu ninachokuamuru leo, 3 cndipo Bwana Mwenyezi Mungu wako atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka mataifa yote kule alikutawanya. 4 dHata kama umefukuziwa katika nchi ya mbali kiasi gani chini ya mbingu, kutoka huko Bwana Mwenyezi Mungu wako atakukusanya na kukurudisha. 5 eYeye Bwana atakurudisha katika nchi iliyokuwa mali ya baba zako, nawe utaimiliki. Naye atakufanya ufanikiwe sana na kukuzidisha kwa idadi kuliko baba zako. 6 f Bwana Mwenyezi Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi. 7 g Bwana Mwenyezi Mungu wako ataweka laana hizi zote juu ya adui zako ambao wanakuchukia na kukutesa. 8Utamtii tena Bwana na kuzishika amri zake zote ninazokupa leo. 9 hNdipo Bwana Mwenyezi Mungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako. Bwana atakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako, 10 ikama ukimtii Bwana Mwenyezi Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukia Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.

Uzima Na Mauti

11 jNinachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza. 12 kHakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?” 13 lWala hakiko ng’ambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?” 14 mLa hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.

15 nTazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo. 16 oNinakuamuru leo kwamba umpende Bwana Mwenyezi Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Bwana Mwenyezi Mungu wako atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.

17Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu, 18 pnakutangazia leo hii kwamba hakika utaangamizwa. Hutaishi maisha marefu katika nchi unayovuka Yordani kuiingia na kuimiliki.

19 qLeo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, 20 rna ili upate kumpenda Bwana Mwenyezi Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa Bwana ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Copyright information for SwhKC